Mazingira ya uwekezaji kwenye nishati kuboreshwa

0
138

Serikali imesema inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji kwenye sekta ya nishati, ili kufungua fursa nyingi za uwekezaji kwenye sekta hiyo.

Kauli hiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akifungua kongamano la nne la kimataifa la Nishati.

Amesema uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji kwenye sekta ya nishati pia utasaidia kufungua fursa kwa wawekezaji wa ndani.

Kongamano hilo linahudhuriwa na wawekezaji pamoja na wafanyabiashara elfu moja kutoka mataifa mbalimbali duniani

Lengo la kongamano hilo linalofanyika kwa muda wa siku mbili ni kufungua milango ya fursa za uwekezaji kwenye sekta ya nishati pamoja na kuzalisha ubia wa uwekezaji.