Max : Vijana wana nafasi kubwa ya kuzuia rushwa

0
149

Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forum, Maxence Melo amesema vijana wana nafasi kubwa ya kupambana na vitendo vya rushwa kwa kupitia mitandao ya kijamii ambayo inakutanisha kundi kubwa la vijana.

Melo amesema hayo wakati akichangia mada kwenye Kongamano la Mapambano dhidi ya Rushwa linalofanyika jijini Arusha.

Ameongeza kuwa kwa sasa dunia imekuwa kama kijiji ambapo taarifa inaweza kusambaa kwa muda mfupi, hivyo ni vema mitandao itumike kama nyenzo mojawapo ya kupambana na rushwa.