Mawaziri wajadili usimamizi wa ziwa Tanganyika

0
151

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema Tanzania ipo tayari kushirikiana na nchi Wanachama wa Usimamizi Endelevu wa ziwa Tanganyika kutekeleza mkataba wa usimamizi endelevu wa ziwa hilo.

Dkt Mpango ametoa kauli hiyo mkoani Kigoma alipokuwa akifungua mkutano wa tisa wa Mawaziri wa nchi Wanachama wa Usimamizi Endelevu wa Ziwa Tanganyika.

Amewataka Mawaziri wanaoshiriki mkutano huo kuutumia kama msingi wa kuongeza makubaliano na ushirikiano, na kuwezesha mamlaka ya usimamizi ya ziwa Tanganyika kuongeza manufaa ya matumizi ya ziwa hilo kwa vizazi vya sasa na baadaye.

Mkutano huo unashirikisha Mawaziri wa Mazingira kutoka Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo pamoja na Zambia.