Mawasiliano kwa njia ya simu Wilaya ya Uyui yaendelea kuimarika

0
194

Mawasiliano ya simu katika kijiji cha Magulyati wilaya ya Uyui mkoani Tabora, yameendelea kuimarika kufuatia ujenzi wa Mnara wa mawasiliano ya simu, utakaotoa huduma kijijini hapo na vijiji jirani.

Akizindua mnara huo uliojengwa na kampuni ya mtandao wa simu ya Airtlel, Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew, amesema Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), imeamua kujenga mnara huo kwa lengo la kuboresha huduma za mawasiliano katika kijiji cha Magulyati na kijiji cha Migongwa, ili kuhakikisha Wananchi wa vijiji hivyo wanapata huduma za mawasiliano ya simu na waweze kujiletea maendeleo na kubadilishana taarifa mbalimbali zinazohusu uchumi, siasa, mila na desturi zao, Utamaduni, Elimu, Biashara, burudani na Michezo.

Uzinduzi wa Mnara huo umehudhuria na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mheshimiwa Kisare Makori ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa, Mbunge wa Jimbo la Igalula Mheshimiwa Venant Protas, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi UCSAF Prof. John Nkoma pamoja na Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Mfuko.