Matukio kwa picha bungeni Februari 4, 2022

0
336

Mkutano wa sita wa Bunge la 12 unaendelea jijini Dodoma ambapo leo kilikuwa ni kikao cha nne cha maswali na majibu kwa wizara mbalimbali.

Aidha, bunge limetengua kanuni ambayo inaelekeza vikao vya bunge kuanza saa tatu asubuhi, ili kuruhusu vikao hivyo kuanza saa nane mchana hadi saa moja jioni kuanzia Februari 7 hadi 18.

Kanuni hiyo imetenguliwa ili muda wa asubuhi kamati za bunge zipate muda wa kufanya vikao vyake, ambavyo havikufanyika kutokana na kujiuzulu kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Hapa chini ni picha mbalimbali za matukio ndani ya ukumbi wa bunge leo;

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akifurahia jambo na Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa (katikati) na Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde (kulia).
Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde (katikati) akiteta jambo na Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega na Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi.
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel akifurahia jambo wakati kikao cha bunge kikiendelea.
Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima akiuliza swali la nyongeza wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni
Wabunge wakiteta jambo huku wengine wakifuatilia kikao cha nne cha mkutano wa sita.
Baadhi ya wabunge wa viti maalum wa CHADEMA wakifuatilia kikao cha bunge
Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi akijibu maswali ya wabunge kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji kwenye majimbo yao.
Wabunge wakiteta jambo wakati kikao cha bunge kikiendelea

Wabunge wakiteta jambo wakati kikao cha bunge kikiendelea
Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee akiuliza swali la nyongeza kuhusu ujezi wa Barabara ya Makongo Juu mkoani Dar es Salaam.
Mbunge wa Makete, Festo Sanga akiuliza swali la nyongeza katika kikao cha bunge.