Mashabiki Yanga wachekelea Masandawana kutolewa

0
313

Huenda mashabiki wa Yanga SC ndio wenye furaha kwa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kuliko hata mashabiki wa Esperance ya Tunisia ambayo ndiyo imeitoa Mamelodi.

Furaha ya mashabiki wa Yanga inatokana na kile wananchoamini kuwa walidhulumiwa goli dhidi ya Masandawana, goli ambalo lingeiwezesha timu yao kufuzu hatua ya nusu fainali.

Masandawana wametolewa kwa jumla ya magoli 2-0 na Esperance kwa kufungwa nje ndani ambayo sasa itacheza fainali dhidi ya Al Ahly ambayo imefuzu baada ya kuitoa TP Mazembe kwa jumla ya magoli 3-0.

Mchezo wa kwanza wa fainali utachezwa Mei 18 mwaka huu na wa pili utachezwa Mei 25, wiki moja baadaye, ambapo ES Tunis itaanzia nyumbani na kumalizia ugenini.

Al Ahly ndiye bingwa mtetezi wa michuano hiyo, na sasa anatafuta kutwaa taji hiyo kwa mara ya pili kama alivyofanya kwenye misimu sita tofauti, ambapo ilitwaa taji hilo mara mbili mfululizo.

Mabingwa hao wa kihistoria wametwaa taji hilo mara 11, na sasa inatafuta la 12, huku Esperance Tunis ikiweka kabati makombe manne ikitafuta nafasi ya kutwaa la tano