Masele kumalizia ujenzi wa Zahanati ya Bushushu

0
213

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele (CCM) ametembelea na kukagua ujenzi wa zahanati ya Bushushu iliyopo katika kata ya Lubaga katika Manispaa ya Shinyanga na kuahidi kupeleka moramu na kutafuta fedha ili kukamilisha ujenzi huo ambao umefikia hatua ya renta.

Masele amefika katika zahanati ya Bushushu ikiwa ni mwendelezo wa ziara katika Jimbo lake kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wajumbe wa kamati za siasa CCM ngazi ya matawi na kata.

“Nimeridhishwa na kasi ya ujenzi wa zahanati ya Bushushu yenye vyumba 15 ambayo mimi mwenyewe niliuanzisha kwa kwa kuchangia mifuko 100 ya saruji.Niwapongeze sana wananchi na wadau mbalimbali kwa ushirikiano wenu kushiriki ujenzi wa zahanati hii” amesema Masele

Mbunge huyo amesema serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya barabara,maji na umeme.