Marufuku michango holela mashuleni

0
126

“Waheshimiwa wabunge wamelalamikia kuwepo utitiri wa michango shuleni. Aidha, Serikali kupitia waraka wa elimu na 5 wa mwaka 2015 na waraka wa elimu namba 6 wa mwaka 2015 imetoa maelekezo bayana kuhusu utekelezaji wa Elimumsingi Bila Malipo ikiwemo matumizi ya fedha za utawala ambazo hutolewa HAZINA na kupelekwa moja kwa moja katika akaunti za shule za msingi na sekondari Nchini kwa ajili ya Vifaa vya kufundishia na kujifunzia, Ukarabati, Uendeshaji wa mitihani ya ndani na Utawala. Asilimia 10 ya fedha hiyo pia hutumika kugharamia huduma za umeme, maji na ulinzi. Hivyo basi, ninaagiza kuwa TAMISEMI kwa kushirikiana na Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri zote nchini kufuatilia matumizi na upatikanaji wa taarifa za matumizi ya fedha hizo pamoja na kuhakikisha hakuna michango holela inayotozwa kwa wanafunzi. Aidha, kuanzia sasa hakikisheni maelezo ya kujiunga na shule za umma (yaani Joining Instructions) yanahakikiwa na kupewa idhini na Katibu Tawala wa Mkoa husika kwa kushirikiana na Maafisa Elimu wa maeneo husika” amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa hotuba ya kuahirisha Bunge.

Tupo mbashara kupitia TBC1, TBC Taifa na mtandao wa YouTube wa TBC online.

Bunge #Bungeni #TBCupdates #TBConline