Waziri wa afya, Ummy Mwalimu amewataka watoa huduma za afya nchini kote kuacha tabia ya kuwatoza fedha wakinamama wajawazito pindi wanavyofika cliniki kupata huduma.
Waziri Ummy ametoa kauli hiyo jijini Tanga mara baada ya kutembelea kituo cha afya cha Makorora na kujionea hali ya utoaji huduma.
“Naomba nisisitize hili si hapa tu bali ni nchi nzima,acheni tabia ya kuwatoza fedha kinamama wajawazito pindi wanapofika cliniki kupata huduma”amesema waziri Ummy
Aidha waziri Ummy ameongeza kuwa serikali itaendelea kuongeza kasi ya usambazaji wa dawa katika maeneo yote ya kutolea huduma za afya hapa nchini.