Marufuku kuuza mafuta kwa magari binafsi

0
224

Sri Lanka imepiga marufuku uuzaji wa mafuta kwa magari yasiyo muhimu, wakati nchi hiyo ikikabiliana na mdodoro mkubwa wa uchumi kuwahi kutokea miongo ya karibuni.

Kwa muda wa wiki mbili zijazo, mabasi, treni, na magari ya kubebea wagonjwa na vyakula ndiyo yatakayouziwa mafuta.

Shuleni nyingi katika maeneo ya mijini zimefungwa, huku watumishi wa umma wakitakiwa kufanya kazi wakiwa majumbani.

Taifa hilo la Kusini mwa Asia lenye watu milioni 22 linaendelea na mazungumzo kuona namna ya kujikwamua kwenye ukata unaosababisha kushindwa kuingiza nishati hiyo na chakula nchini humo.

Uchumi wa Taifa hilo umeathiriwa kwa kiasi kikubwa na janga la UVIKO19, kupanda kwa bei ya mafuta na kupungua kwa mapato ya serikali kutokana na kufutwa kwa baadhi ya kodi.