Marobota 170 ya vitenge yakamatwa Tanga

0
209

Mkuu wa mkoa Tanga, Omary Mgumba amewataka baadhi ya viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo kujitathimini.

Mgumba ametoa kauli hiyo jijini Tanga kufuatia kukamatwa kwa marobota 170 ya doti za vitenge, yaliyoingia nchini kwa kutumia majahazi pasipo kufuata utaratibu.

Marobota hayo yamekamatwa wilayani Mkinga kufuatia taarifa zilizotolewa na raia wema.

Tayari mkuu huyo wa mkoa wa Tanga amezungumza kwa njia simu na mmliki wa marobota hayo ya doti za vitenge na kumtaka afike jijini Tanga akiwa na nyaraka halali za shehena hiyo.