Marais wastaafu wa Tanzania wakabidhiwa tausi 100

0
564

Rais John Magufuli amewakabidhi marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tausi 25 kila mmoja, ambapo Mama Maria Nyerere amepokea tausi hao kwa niaba ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Rais Magufuli amewakabidhi marais wastaafu tausi mkoani Dodoma ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wao wa namna walivyowatunza walipokuwa madarakani.

Akikabidhi tausi hao Rais Magufuli amesema Tanzania haikuwahi kuwa na tausi, lakini waliletwa na Hayati Baba wa Taifa na baadaye Marais wote waliofuata waliwatunza vizuri.

Akizungumza kwa niaba ya marais wastaafu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa awamu wa pili Mzee Alli Hassan Mwinyi na Rais wa awamu ya tatu, Mzee Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete amemshukuru Rais Magufuli kwa kuendelea kuwathamini na kuwapatia tausi hao ambao walikuwa wakiwatamani kwa muda mrefu.