Mapokezi ya wajumbe wa Sekretarieti ya CCM

0
275

Hali ilivyo katika ofisi ndogo ya Chama Cha Mapinduzi, Lumumba jijini Dar es Salaam wakati wa mapokezi ya Wajumbe wa Sekretarieti ya chama hicho, leo Aprili 5, 2024.

Itakumbukwa kwamba kikao maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichoongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni kilifanya mabadiliko ya wajumbe wa nafasi mbalimbali.

Wajumbe waliofika ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Amos Makalla; Katibu Mkuu wa UVCCM, Jokate Mwegelo; Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi, Ally Hapi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Mongella.