Maonesho makubwa ya kahawa yamefanyika nchini Japan, ambapo watumiaji wengi wa kahawa nchini humo wamejitokeza kuonja kahawa ya Tanzania.
Maonesho hayo ya kahawa yanaelezwa kuwa ni muhimu katika kuendelea kukuza soko la kahawa ya Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Japan, Baraka Luvanda amewaongoza maafisa wa ubalozi wa Tanzania humo, maafisa wa bodi ya Kahawa Tanzania pamoja na watu mbalimbali katika maonesho hayo.
Maonesho hayo yamefanyika katika kituo cha kimataifa cha maonesho cha
Tokyo Big Sight.
Japan ni miongoni mwa nchi zenye wanywaji wengi wa kahawa duniani.