Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Taaluma), Profesa Bonaventura Rutinwa amewataka watayarishaji wa vipindi vya elimu kwa umma kutumia mafunzo waliopatiwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutengeneza vipindi vyenye maslahi ya Taifa.
Prof. Rutinwa akihitimisha mkutano wa mafunzo ya siku tano ya watayarishaji wa vipindi vya elimu kwa umma jijini Arusha, amewataka waelimishe umma kuhusu miradi inayoendelea hivi sasa kupitia taasisi zao.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Redio wa TBC, Aisha Dachi amesema washitiri wamejengewa uwezo wakutayarisha vipindi bora.
Moja ya washiriki amesema anaamini watatumia mafunzo waliyopata kuleta mabadiliko katika majukumu yao ya kuelimisha jamii.
“Tutafanya mabadiliko makubwa kuandaa vipindi bora na kutumia vizuri mitandao ya kijamii pamoja na kutangaza shughuli zinazofanywa na taasisi zetu,” amesema.
Wadhamini wakuu wa mafunzo hayo ambao ni UDSM wamesema mafunzo yanayotolewa na TBC kwa washitiri ni muhimu kutokana na kuelimisha jamii.
Mkutano wa mafunzo wa 106 wa watayarishaji wa vipindi vya elimu kwa umma unatarajiwa kufanyika mkoani Mwanza mwaka 2022.