Maofisa Habari watakiwa kuzingatia ubora wa vipindi

0
116

Meneja wa Huduma za Televisheni wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Victor Elia akitoa mada ya uandaaji wa vipindi vya Televisheni kwenye mkutano wa 106 wa mafunzo ya watayarishaji wa vipindi vya Televisheni Redio na Mitandao ya Kijamii.

Victor Elia amesisitiza watayarishaji wa vipindi kuzingatia misingi ya uandaaji wa vipindi hivyo ili kuepuka kuandaa vipindi ambayo havina ubora na viwango kwaajili ya kuhabarisha Umma.

Baadhi ya misingi hiyo ni pamoja na kuwa na wazo la kipindi ambacho kinatakiwa kuzalishwa, kuandaa mazingira ya kufanyia kipindi yanayoendana na mada husika, kuwa na mgawanyo wa majukumu katika kuandaa kipindi husika.

Mafunzo hayo yameandaliwa na TBC ambayo yanajumuisha Maofisa wa Habari wa Wizara Taasisi Mashirika ya Umma, Idara na Halmashauri.