Maofisa AICC wasimamishwa kazi

0
394

Uongozi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kimewasimamisha kazi kupisha uchunguzi wakurugenzi watatu na maofisa wengine waandamizi watatu.

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano cha AICC, imesema kuwa wakurugenzi hao wamesimamishwa kazi kwa tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kukiuka taratibu na kanuni za uendeshaji wa mashirika ya umma.

Waliopumzishwa kazi ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Mkurugenzi wa Mikutano na Masoko, Mkurugenzi wa Miliki na Miradi pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu na Utawala. Wengine ni Mhasibu Mkuu pamoja na Meneja wa AICC.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, umma utajulishwa kuhusu hatua nyingine za uchunguzi huo unaofanywa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.