Manispaa ya Ilemela yafanikiwa kuongeza makusanyo ya mapato

0
242

Halmashauri ya manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, imefanikiwa kuongeza mapato yake kwa zaidi ya shilingi Bilioni nne mwaka 2015 hadi kufikia zaidi ya shilingi bilioni tisa mwaka 2020.

Ongezeko hilo la mapato limetokana na matumizi sahihi ya mfumo wa elektroniki,uadilifu na nidhamu ya utendaji kazi miongoni mwa watumishi wa halmashauri hiyo.

Akizungumza katika hafla ya kuwaapisha madiwani 27 wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela, mbunge wa jimbo hilo Dkt.Angelina Mabula amesema ni muhimu kuendelea kutumia mfumo wa kielektroniki ili kukusanya fedha nyingi zaidi, zitakazorahisisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.PAUSE

Naye mkuu wa wilaya ya Ilemela, Dkt.Severin Lalika amesema serikali itashirikiana vyema na madiwani hao ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi kwa kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.