Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika halmashauri ya Nanyumbu mkoani Mtwara, umekamilisha ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 1.8 na kufunga taa 40 kwenye barabara hiyo.
Barabara hiyo imejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni moja, fedha ambazo ni tozo ya mafuta ambazo zilitolewa na serikali katika mwaka wa fedha 2021/2022.
Barabara hiyo ni ya kwanza kujengwa katika mji wa Mangaka uliopo katika halmashauri ya Nanyumbu toka uanzishwe mwaka 2007 na kuweka historia ya kuwa na barabara ya lami.
“Mji wa Mangaka haujawai kuwa na hata kilomita moja ya barabara ya lami kwa maana ya upande wa barabara zinazosimamiwa na TARURA, hii ndiyo lami ya kwanza.” amesema Mhandisi Hussein Mwombeki,
Meneja wa TARURA Nanyumbu
Amesema katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 serikali ilitoa shilingi bilioni 2.4 na kati ya hizo shilingi bilioni moja ni za tozo ya mafuta.