Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amemuagiza Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana kuhakikisha mamlaka zote zinazosimamia utalii nchini zinaacha urasimu wa utoaji vibali kwa wawekezaji, ili sekta ya utalii ipige hatua zaidi.
Makamu wa Rais amesema wadau wanaoomba vibali mara nyingi hukutana na urasimu kwenye mamlaka mbalimbali, hali inayokwamisha ukuaji wa sekta hiyo.
“Kumekuwa na urasimu huko kwenye utoaji vibali, Waziri wa Maliasili upo hapa naomba ukashughulikie hili, urasimu ukomeshwe kwenye mamlaka za utalii.” ameagiza Dkt. Mpango
Katika hatua nyingine Dkt. Mpango ameiomba wizara ya Maliasili na Utalii kuangalia viingilio rafiki hasa kwa wazawa, ili iwe rahisi kwao kutembelea hifadhi mara kwa mara.
Dkt. Mpango alikuwa akizungunguza wakati wa hafla ya kukabidhi malori kwa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) toka mradi wa Regrow.