Mamia ya watu wakiwemo viongozi mbalimbali, wamejitokeza katika mazishi ya aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika serikali ya awamu ya tatu, Idd Simba aliyefariki Dunia hapo jana katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Mazishi ya Marehemu Idd Simba yamefanyika katika Makaburi ya Mwinyi Mkuu Magomeni jijini Dar es salaam.
Viongozi waliohudhuria mazishi ya Mzee Idd Simba ni pamoja na Marais Wastaafu Mzee Benjamin Mkapa na Dkt Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt Mohamed Gharib Bilal na Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Abdulrahman Kinana.
Marehemu Idd Simba aliyezaliwa Oktoba Nane mwaka 1935, amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini.