Mamia wajitokeza kumzika Askofu Mwenisongole

0
131

Mazishi ya Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa la Assemblies of God Tanzania (TAG) Dkt. Ranwell Mwenisongole yanaendelea hivi sasa katika makaburi ya Ichenjezya Mama wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Awali ilifanyika ibada ya mazishi iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa TAG, Dkt, Barnabas Mtokambali, ibada iliyofanyika katika uwanja wa CCM Vwawa.

Dkt. Mwenisongole ambaye alikuwa Askofu Mkuu wa pili wa Kanisa la Assemblies of God Tanzania, alifariki dunia tarehe 25 mwezi huu katika hospitali ya Lugalo mkoani Dar es Salaam.