Mambo manne ya kufanya katika Siku ya Kimataifa ya Watu Wazee 2020

0
531

Historia

Desemba 14, 1990, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (kwa azimio la 45/106) liliteua Oktoba Mosi kuwa Siku ya Kimataifa ya Wazee.

Hii ilitanguliwa na mipango kama vile mpango wa utekelezaji wa Vienna juu ya kuzeeka ambao ulipitishwa na Bunge la Ulimwengu la 1982 juu ya kuzeeka na kupitishwa baadaye mwaka huo na Baraza Kuu la UN.

Mnamo 1991, Mkutano Mkuu (kwa azimio la 46/91) ulipitisha Kanuni za Umoja wa Mataifa kwa wazee. Mwaka 2002, Bunge la Pili la Ulimwengu juu ya kuzeeka lilipitisha Mpango wa Kimataifa wa Utekelezaji wa Madrid juu ya kuzeeka, kujibu fursa na changamoto za kuzeeka kwa idadi ya watu katika Karne ya 21 na kukuza maendeleo ya jamii kwa miaka yote.

Siku ya Kimataifa ya Wazee 2020
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka 2020 ni “Familia na Jamii Ishiriki Kuwatunza Wazee.”

Mbinu za kuboresha uhusiano mzuri na wazee

  1. Kuwa na ujuzi mzuri wa mawasiliano
    Wakati watu wako karibu na kila mmoja kwa miaka, ni rahisi kuanguka katika tabia mbaya za mawasiliano. Saidia mpendwa wako kudumisha uhusiano bora kwa kujifunza kuwasiliana na kufanya mazungumzo na mzee wako.
  2. Kuandaa hafla za kifamilia
    Wazee wengi huwapa wanafamilia wao kipaumbele chao cha kwanza kabisa hivyo mkusanyiko wa wanafamili mara kadhaa kwa mwaka husaidia kuonesha upendo kwa wazee na vizazi vyote tofauti viweze kuunganishwa pamoja.
  3. Sherehe tarehe muhimu
    Kushiriki wakati wa furaha pamoja hujenga uhusiano mzuri na wazee wetu. Weka alama tarehe muhimu ya mzee wako kwenye kalenda, na usherehekee tarehe hizi kwa kumpeleka kwenye chakula cha mchana cha kuzaliwa au kumwalika kwa chakula cha jioni. Kama yupo mbali unaweza kutumia hela au hata kumpigia simu na kumtakia siku njema ya siku husika.

Vilevile msaidie mpendwa wako kupanga mikusanyiko ya kijamii na shughuli na marafiki kujenga kumbukumbu ambazo zinajaza siku zake na furaha.

  1. Shiriki katika kutunza afya yake
    Kutokana na umri wazee kuhitaji uangalizi wa karibu, ni muhimu kuhakikisha unafatilia na kusaidia katika kuimarisha afya za wazee. Pia kumsaidia kufanya mzoezi na kuanda mlo mzuri unaoendana na mahitaji ya mwili wake

Zingatia ubora sio wingi wa matendo wazee wanapaswa kuwa na mawasiliano ya kijamii mara kwa mara ili kuhakikisha hawajisikii kutengwa, lakini ni muhimu pia kuhakikisha mawasiliano hayo yana maana na yanafaida kwao.