Mamba watafutwe na wavuliwe

0
357

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego amefika katika Kata ya Migoli na kuagiza kuvuliwa kwa mamba katika Bwawa la Mtera, ikiwa ni siku chache baada ya kuripotiwa taarifa ya mvuvi kuuawa na mamba na watu wengine zaidi ya wanne kujeruhiwa katika bwawa hilo, jambo ambalo limekuwa tishio kwa usalama wa wananchi.

Dendego amesema hayo baada ya kuonana na wananchi waliojeruhiwa na kuitaka Mamalaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) kuhakikisha inashirikiana na wananchi kuwavua mamba hao.

Aidha, amesema katika mwaka wa fedha ujao Serikali itatenga fedha kwa wananchi wa kata hiyo na wanaozunguka bwawa hilo kwa ajili ya ununuzi wa boti za kisasa ambazo zitawasaidia wavuvi katika shughuli zao.