Makonda apokea msaada wa Milioni 27 kusaidia vita dhidi ya Corona

0
344

Jumuiya ya Dawoodi Bohora Tanzania leo imekabidhi vifaa mbalimbali vya kujikinga na corona vyenye thamani ya Shilingi Milioni 27 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwa lengo la kuwakinga wananchi wa Mkoa huo.

Akipokea Vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dr. Rashid Mfaume amesema miongoni mwa vitu vilivyotolewa ni pamoja na Vifaa vya kuzuia maambukizi, vifaa vya kinga binafsi, vyakula vya kujenga mwili, sabuni, dawa za kunawa mikono na mashine za kuua mazalia ya bacteria.

Aidha Dr. Mfaume amesema vifaa hivyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona ambapo amewataka wananchi kuendelea kuchukuwa tahadhari na kufuata kanuni na maelekezo yanayotolewa na Wizara ya Afya.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Jumuiya ya Mabohora Murtaza Adamjee amesema Jumuiya hiyo itaendelea kuunga mkono Juhudi za Serikali ya Mkoa huo katika mapambano dhidi ya Corona ambapo pia wameipongeza Serikali kwa jitihada wanazozifanya kukabiliana na corona.