Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amekagua maandalizi na marekebisho ya uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha, uwanja uliopangwa kufanyika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2024.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika ukaguzi huo wa uwanja Makonda aliongozana na viongozi mbalimbali akiwemo Tumaini Nyamhokya ambaye ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania pamoja na Makamu wake.
Nyamhokya amewaambia waandishi wa habari mkoani Arusha kuwa maandalizi ya sherehe za Mei Mosi yanaendelea vizuri na kila kamati inafanya kazi yake kikamilifu ili kuhakikisha sherehe hizo zinakuwa nzuri na za kuvutia.