Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ametoa rai kwa Watanzania kuendelea kutumia teknolojia mbalimbali za ubunifu katika shughuli za kijamii na maendeleo ili kuongeza fursa za kiuchumi.
Profesa Mkenda amesema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wiki ya kitaifa ya ubunifu pamoja na uzinduzi wa mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU ) kwa mwaka huu.
Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufunguliwa tarehe 16 mwezi huu na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi jijini Dodoma.
Maadhimisho hayo yatakayoongozwa na kauli mbiu ya ubunifu kwa maendeleo endelevu, yatafikia kilele chake tarehe 19 mwezi huu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.