Makatibu Mahsusi watakiwa kutunza siri za serikali

0
147

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Makatibu Mahsusi nchini kitekeleza majukumi.yao kwa kuzingatia weledi na kuwa waadilifu.

Ametoa wito huo jijini Dodoma wakati akifungua rasmi mkutano wa tisa wa kitaaluma wa Makatibu Mahsusi.

Rais Samia amewataka Makatibu Mahsusi nchini kuacha kutoa siri ama nyaraka za serikali, kwani hilo ni kosa kubwa kwenye utumishi wa umma.

Amefafanua kuwa siri nyingi za serikali zimekuwa zikisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, jambo linaloonyesha baadhi ya Makatibu Mahsusii si waaminifu.

Kwa mujibu wa Rais Samia Suluhu Hassan, kada hiyo imepewa jina la Makatibu Mahsusi kwa kuwa wao ni mahususi na kwamba kama atakayetokea na kujiona sio mahususi basi yeye ni mpiga chapa.

Amewataka kujiheshimu, kuheshimu sehemu zao za kazi na sehemu za kazi za wengine.

Rais Samia Suluhu Hassan amewapongeza Makatibu Mahsusi nchini kwa kazi kubwa ambayo wamekuwa wakiifanya na kuongeza kuwa ufanisi wa viongozi mbalimbali unawategemea wao.