Uzinduzi wa Tawi la Benki ya Biashara ya Mkombozi jijini Dodoma umefanyikia leo hii
Makamu wa Rais Samia Suluhu amesema Tanzania imepiga hatua katika upatikanaji wa huduma jumuishi za kifedha, ambapo kiwango cha huduma rasmi za kifedha umefikia asilimia 65 huku utumiaji wa huduma isiyo rasmi ikiendelea kupungua.
Tawi la Mkombozi jijini dodoma imefanya jiji la dodoma kuenedela kufunguka kibiashara na kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.
hata hivyo makamu rais amebaini kuwa asilimi 28 ya watanzania hawatumii huduma za kibenki hasa wa vijijini kutokana na kutofikiwa na huduma hizi
Aidha amewataka wananchi kuachana na utaratibu wa zamani wa kutunza fedha majumbani
Naye kaimu mkurugenzi mtendaji wa benki ya biashara ya mkombozi Thomas Enock ameeleza jinsi benki hiyo inavyounga mkono serekali ya awamu ya tano