Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani kitafanyika mkoani Simiyu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amesema maadhimisho hayo yatatanguliwa na maonesho ya wajasiriamali yatakayodumu kwa siku saba
Mtaka amesema pamoja na kuwa mgeni rasmi, Makamu wa Rais anatarajiwa kuwa na ziara ambapo atazindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi mbalimbali mkoani humo
Maadhimisho wa siku ya wanawake duniani yanaendelea katika mikoa mbalimbali na kilele chake ni Machi 8 kauli mbiu ikiwa ni kizazi cha usawa kwa maendeleo ya Tanzania ya sasa na ya baadaye.