Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo uchumi wake unatoa fursa

0
158

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo uchumi wake unatoa fursa ya kupata mikopo kwenye taasisi za kimataifa, hivyo itakopa kwa ajili ya maendeleo na sio kinyume na hapo.

Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uwasilishwaji wa taarifa kuhusu Matumizi ya Fedha za Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO -19, Dkt. Mpango amesema kwa mujibu wa taarifa ya Benki ya Dunia ya Mwezi Oktoba mwaka 2021, Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake upo imara na inakopesheka na haiko katika kundi la nchi zisizokopesheka

Makamu wa Rais ameleezea kuwa, mkopo wa shilingi Trilioni 1.3 uliotolewa na Shirika la fedha la Kimataifa (IMF) kwa Tanzania umekuwa na tija kubwa, na kwamba utasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa Wananchi.