Makamu wa Rais Dkt, Philip Isdor Mpango ametoa maelekezo ya kuboresha michezo ya SHIMIWI leo Oktoba 23, 2021 mjini Morogoro wakati akifanya ufunguzi rasmi wa michezo hiyo
Amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo na Uongozi wa SHIMIWI wa kurejesha mashindano hayo kufuatia maelekezo ya Serikali yaliyotolewa na Waziri Mkuu hivi karibuni ya kutaka michezo hiyo ifufuliwe.
Aidha, Katibu Mkuu wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbasi ambaye amezungumza kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana ya michezo amemshukuru Makamu Rais kwa kukubali kuwa mgeni rasmi na kuja kufungua mashindano hayo kwa niaba ya Rais ambapo ametumia fursa hiyo kufafanua mafanikio lukuki yaliyopatikana kwenye sekta ya michezo katika kipindi kifupi cha Serikali ya Awamu ya Sita.
Katika mashindano ya mwaka huu Wizara 24, Mikoa 11 Wakala 4 na Idara 8 za Serikali zimeshiriki.