Makamu wa Rais amuwakilisha Rais Magufuli mkutano wa SADC

0
545

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameondoka nchini leo kwenda Gaborone nchini Botswana kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa dharura wa SADC-TROIKA kuhusu ulinzi eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kwenye mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali, Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli.

Mkutano huo wa dharura unaotarajiwa kufanyika Novemba 28 mwaka huu jijini Gaborone umeitishwa kwa ajili ya kujadili hali ya siasa, ulinzi na usalama katika jumuiya hiyo.

Aidha, mkutano huo pia utaangazia changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika eneo la siasa, ulinzi na usalama na pia kwa pamoja kuweza kupata utatuzi wa mambo yatakayobainishwa kwenye mkutano huo.