Makalla kutatua kero jimbo kwa jimbo

0
204

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla anatarajiwa kuanza ziara ya kusikiliza na kutatua kero pamoja na changamoto za Wananchi wa mkoa huo jimbo kwa jimbo, ikiwa ni mpango wake wa kupatia ufumbuzi kero za Wananchi.

Makalla amesema ziara hiyo itaanza rasmi Jumatatu Agosti 30 kwenye jimbo la Kawe viwanja vya Tanganyika Packers, Agosti 31 jimbo la Kibamba, Septemba Mosi jimbo la Segerea, Septemba 2 jimbo la Mbagala na Septemba 3 jimbo la Kigamboni.

Aidha Makalla amesema kutakuwa na jopo la Wataalamu wabobezi wakiwemo Watendaji wa Serikali, Wanasheria, Kamishina wa Ardhi, Maafisa Ardhi, Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) na wadau wote wanaojihusisha na masuala ya kisheria.

Makalla ametoa wito kwa Wananchi wote wenye migogoro kutumia fursa hiyo kuwasilisha malalamiko yao, ili yaweze kupatiwa ufumbuzi kwa mujibu wa sheria.