Nyasi kutumika kutengeneza mbao

0
302

Kampuni iitwayo Plantd imefanikiwa kubuni mbao zinazotokana na nyasi

Kampuni hiyo hivi karibuni imetambulisha suluhisho la kudumu la kufyonza hewa ukaa [Carbondioxide] kupitia nyasi hizo.

Mmea wa nyasi hizo unakuwa kwa haraka unaweza kufikia kimo cha futi 20-30 ndani ya mwaka mmoja hivyo kuonekana ni mmea bora kutumika kama mbadala wa miti kwaajili ya kutengenza mbao.

Nyasi hizo huoteshwa mara moja tu na kudumu kila msimu huku zikiwa na sifa kubwa ya kuhifadhi hewa ukaa [CO2] kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko miti.

Kutokana na sifa hiyo nyasi hizo zinaaminika kuwa na kasi ya kupunguza madhara yanayosababishwa na ongezeko la joto duniani kulinganisha na njia za asili.

Wataalamu wa ujenzi wamejaribu kutumia nyasi hizo kutengeneza zana za ujenzi ambazo zimeonekana kuwa imara na bora zaidi kuliko mbao ya mti.

Katika chapisho la Forbes imeripitiwa kuwa teknolojia hiyo ya nyasi imeleta mageuzi makubwa katika matumizi ya miti kutengeza mbao kwani nyasi hizo zimekuwa mbadala wa mbao za miti kwenye ujenzi wa nyumba kwakuwa ni njia yenye gharama nafuu na imara zaidi.

Mbao zinazotokana na nyasi hizo zinaweza kutumika kupaua nyumba, kuezeka paa, kutumika kama ukuta wa nyumba na hata kutumika kama sakafu.