Makabila 3 ya mbu wasumbufu Tanzania

0
219

Wanasayansi wa Taasisi ya Afya Ifakara iliyopo wilayani Kilombero mkoani Morogoro wamesema, kuna makabila zaidi ya 300 ya Mbu duniani, lakini ni makabila matano tu ya mbu hao ndio yana usumbufu zaidi kwa nchi za Bara la Afrika.

Wakizungumza na mwandishi wa TBC, wanasayansi hao wazawa wamesema kati ya makabila hayo matano imeonekana kuwa makabila matatu ndio yanayosumbua sana Tanzania kwa kusambaza ugonjwa wa malaria.

Wamesema kwa Tanzania ugonjwa wa malaria unasumbua sana watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano na akina mama wajawazito, hivyo wameanza kutumia ndege zisizo na rubani kutafuta mazalia ya mbu hao hasa katika ukanda wa bonde la mto Kilombero.

Wamesema njia hiyo itawawezesha kutambua maeneo yote yenye mazalia ya mdudu hao ili kufanya tafiti zitakazokuja na majibu ya kukabiliana nao.

Hatua hiyo inafuatia malalamiko ya wananchi wengi kuugua malaria katika ukanda huo.