Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza majeruhi wote wa ajali iliyohusisha magari manne katika eneo la Ngaramtoni mkoani Arusha waliolazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Mount Meru wapatiwe matibabu bila ya kulipia gharama yoyote.
Akiwajulia hali majeruhi wa ajali hiyo Dkt. Mollel amesema, wote wanaendelea vizuri na mmoja amepatiwa rufaa ya kwenda hospitali ya Rufaa ya Kanda KCMC Moshi mkoani Kilimanjaro.
Aidha, Dkt. Mollel ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Arusha na Watanzania wote kuwa watulivu wakati majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu.
Kwa wale waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo Dkt. Mollel amesema, utaratibu wa kupatiwa miili unaandaliwa.