Majaliwa : Tumieni Mwezi Mtukufu kuliombea Taifa

0
149

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasisitiza waislam nchini watumie Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuibariki Tanzania, viongozi na wananchi wake wadumishe amani na mshikamano.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasisitiza Waumini wa dini ya Kiislam nchini kutumia mwezi Mtukufu wa Ramadhani kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuibariki Tanzania, pamoja na Viongozi na Wananchi ili wadumishe amani na mshikamano.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema.hayo mkoani Dar es salaam wakati wa fainali za mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur’an yaliyohusisha Washiriki 15 kutoka nchi 11.

Pia ametoa rai kwa Waumini wa dini ya Kiislam nchini kuendelea kuyaishi mafundisho wanayoyapata katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

“Natambua mchango mkubwa wa waumini katika kuienzi na kuitunza amani kwa kufuata miongozo ya Viongozi wetu kupitia mafundisho ya Qur’an ambayo hututaka kuepuka kuivuruga amani,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Amesema amani ni matokeo ya msingi imara ulioachwa na Waasisi wa Taifa, hivyo haina budi kuienzi na kuilinda kwa ajili ya maslahi na mustakabali wa Taifa.

Waziri Mkuu Majaliwa ameongeza kuwa, ni vema vijana hao waliohifadhi Qur’an wakaendelezwa kitaaluma katika fani zingine za elimu, kwani uwepo wao ni muhimu katika kujenga jamii bora na yenye uadilifu.

Ameyasema hayo leo katika Fainali za Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur’an yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yanahusisha washiriki 15 kutoka nchi 11.

Pia, Waziri Mkuu ametoa rai kwa waumini wa dini ya kiislam nchini waendelee kuyaishi mafundisho wanayoyapata katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwenye maisha yao ya kila siku.

“Natambua mchango mkubwa wa waumini katika kuienzi na kuitunza amani kwa kufuata miongozo ya viongozi wetu kupitia mafundisho ya Qur’an ambayo hututaka kuepuka kuivuruga amani.”

Amesema amani ni matokeo ya msingi imara iliyoachwa na waasisi wa Taifa, hivyo hawana budi kuienzi na kuilinda kwa ajili ya maslahi na mustakabali wa nchi. “Mwitikio mkubwa tunaouona kwenye mashindano haya ni kielelezo cha amani, umoja na mshikamano tulionao.”

Pia, Waziri Mkuu amesema ni vema vijana hao waliohifadhi Qur’an wakaendelezwa kitaaluma katika fani zingine za elimu kwani uwepo wao ni muhimu katika kujenga jamii bora na yenye uadilifu.