Majaliwa : Makatibu Tawala ni kiungo muhimu kati ya Serikali na Wananchi

0
205

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Makatibu Tawala walioapishwa hii leo, kutambua kuwa wao ni kiungo muhimu baina ya Serikali na Wananchi, katika kuwaletea maendeleo Wananchi hao.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo Ikulu Chamwino mkoani Dodoma wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Makatibu Tawala walioteuliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema kuwa wakati wakitekeleza majukumu yao, Makatibu Tawala hao wajue kuwa Serikali inataka kuona miradi ya maendeleo iliyoanzishwa inawafikia Wananchi.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Majaliwa, kitu cha kwanza wanachokiwa kukifanya kwa umakini Makatibu Tawala hao  ni kusimamia miradi ya maendeleo iliyo katika wilaya mbalimbali, ambayo ina umuhimu mkubwa kwa Wananchi.