Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kushuhudia uchepushaji wa maji kesho Novemba 18, 2020 kutoka Mto Rufiji kwa ajili ya kuzalisha umeme katika Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (Julius Nyerere Hydro Power Project) katika eneo la Stiegler’s Gorge.
Uchepushaji wa maji utapita kwenye handaki kwa lengo la kupisha ujenzi wa tuta kuu la Bwawa la Julius Nyerere.
Baadhi ya wageni watakaohudhuria hafla hii ni pamoja na Waziri wa Umeme na Nishati Mbadala kutoka Misri, Dkt. Mohamed Shaker Elmarkabi akiongozana na Waziri wa Nyumba wa nchi hiyo, Dkt. Asim Abdelhamid Hafiz Elgazar pamoja na viongozi waandamizi wa serikali ya Tanzania.
Pichani ni mafundi wakiendelea na kazi katika mradi huo wa kuzalisha umeme.