Majaliwa aunguruma mirerani

0
176

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa siku kumi na tano kwa Wizara ya madini kupitia na kufanya marekebisho ya kanuni za uuzaji na uchakataji wa madini ya Tanzanite.

Waziri Majaliwa ametoa agizo hilo wakati wa hafla ya kuzindua kituo cha pamoja Cha Tanzanite Magufuli (Magufuli Tanzanite One Stop Center) kilichopo Mirerani Mkoani Manyara.

Majaliwa amebainisha kuwa kurekebishwa kwa kanuni ya biashara ya madini ya Tanzanite itasaidia kujenga heshima ya nchi kupitia eneo la Mirerani ambalo linazalisha madini hayo.

Waziri Majaliwa pia ametoa miezi mitatu kwa wachakataji, wauzaji na wanunuzi wa madini ya Tanzanite nchini kufanya mpango wa kujipatia maeneo nakujenga ofisi zao eneo la Mgodi huo kama sehemu ya kuitangaza nchi kwa mataifa mengine.