Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa ameanza ziara ya kikazi mkoani Mbeya ambapo ametembelea shamba la mwekezaji wazao la parachichi na kuwaagiza maafisa kilimo na ughani kuhakikisha wanatembelea wakulima wadogo wa zao hilo ili kuwapa elimu na kuwawezesha kuongeza kasi ya uzalishaji
Akiwa katika shamba la mwekezaji huyo, Kuza Afrika, Waziri Mkuu amesema uwekezaji huo uliofanywa ni mkubwa unapaswa kuungwa mkono na serikali na kuwataka wakulima kuzalisha kwa wingi ili wauze kwa mwekezaji huyo
Majaliwa pia ametoa ahadi ya kushughulikia migogoro ya wakulima wa chai wilayani Rungwe kwa kuwakutanisha vyama vya ushirika na baadhi ya wakulima wa chai
Wakati hi huohuo amesema serikali imefikia hatua za mwisho za kidiplomasi katika kujadili kurudisha soko la nchini Afrika Kusini ili kuuza matunda katika nchi hiyo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amewahakikishia wakulima wa zao la parachichi kuwa serikali itaanza uzalishaji wa miche mingi itakayotolewa kwa wakulima ili kulipa thamani zao hilo.