Mahakama Kuu ya Tanzania Januari 14 inatarajia kutoa maamuzi dhidi ya shauri lililofunguliwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe na wenzie ya kupinga muswada wa mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa kujadiliwa bungeni
Mahakama hiyo imesikiliza pingamizi la Serikali dhidi ya shauri la muswada wa Sheria ya marekebisho ya vyama vya Siasa wa mwaka 2018 chini ya Jaji Benhajji Masoud.
Pingamizi la serikali liliwasilishwa na Jopo la mawakili wa serikali wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Mark Mulwambo ambaye amedai kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania haina mamlaka ya kusikiliza shauri la kupinga muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Vyama vya Siasa.
Kwa upande wa walalamikaji wamedai kuwa Katiba inaipa mamlaka mahakama ya
kusikiliza shauri hilo kwa sababu inatoa nafasi kwa mtu yeyote kupekea kesi
pindi anapoona haki yake au katiba inavunjwa .