Mahakama Afrika Kusini yazuia ndege ya ATCL

0
207

Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) imezuiliwa kuondoka nchini Afrika Kusini kwa amri ya Mahakama Kuu ya Gauteng,- Johannesburg.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe na kusainiwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo anayeshughulikia Uchukuzi Dkt Leonard Chamuriho imesema kuwa, Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu inafuatilia suala hilo ili ndege hiyo iachiwe.

Katika taarifa hiyo, Waziri Kamwelwe ameomba radhi kwa usumbufu ulijitokeza kwa abiria wa ATCL waliokuwa wakisafiri kutoka Johannesburg kwenda jijini Dar es Salaam.

Waziri ameomba radhi kutokana na abiria hao kushindwa kusafiri kutoka uwanja wa Oliver Tambo jijini Johannesburg baada ya ndege hiyo kushindwa kufanya safari kama ilivyopangwa kutokana na kuzuiwa.