Mtu mmoja amefariki dunia na kaya zaidi ya 150 hazina makazi baada ya nyumba zao kusombwa na maji wilayani Kilosa mkoani Morogoro, kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mto Wami kujaa maji na kupoteza uelekeo.
Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka amesema tayari wameanza kufanya tathmini ya madhara yaliyosababishwa na maji hayo pamoja na kutoa msaada kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko.
Amesema kujaa kwa mto Wami kumesababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya Manyara, Singida na Dodoma.
Baadhi ya Wananchi wa Kilosa wamesema mafuriko hayo yalitokea majira ya saa tisa usiku wa kuamkia leo Desemba 5, 2023.