Mafunzo kwa bodi ya wakurugenzi TBC

0
158

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha akitoa mafunzo kwa wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo, mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT) kwa lengo la kuwajengea uwezo katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Mafunzo hayo yatakayofanyika kwa muda wa siku mbili, yamefunguliwa rasmi hii leo na Mwenyekiti wa bodi hiyo Stephen Kagaigai.

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania ilizinduliwa rasmi Oktoba 6 mwaka huu na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye.