Maduka kumi yateketea kwa moto Karagwe

0
274

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kagera kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola, linaendelea kufanya tathmini ya mali zilizoteketea katika maduka Kumi, kufuatia ajali ya moto iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika mji mdogo wa Kayanga wilayani Karagwe ambayo chanzo chake bado hakijajulikana.

Kamanda wa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kagera, Khamis Dawa amekiri askari wa vikosi vya uokoaji kuchelewa kufika katika eneo la tukio kutokana na jiografia ya mkoa huo na kulazimika kutumia zaidi ya saa mbili kufika katika eneo la tukio wakitokea mjini Bukoba.

Moto huo ulioanza majira ya saa tano usiku ambao bado haujajulikana chanzo chake, umeteketeza jengo moja lililokuwa na maduka linalomilikiwa na Nehemia Kazimoto.