Kufuatia mlipuko wa virusi vya corona, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amewaagiza walimu wa madrasa zote nchini kufunga madrasa hizo mpaka hapo utaratibu mpya utakapotolewa.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, mufti amewataka waumini wa dini ya Kiislamu kutii na kutekeleza maagizo yanayotolewa na serikali ikiwa ni pamoja na kuepuka mikusanyiko.
Aidha amewataka waumini wote kuhakikisha wanachukua udhu nyumbani kabla ya kwenda msikitini.