Madiwani Morogoro waaswa kusimamia usafi

0
274
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo amewaagiza madiwani wa kata za Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuimarisha usafi katika kata zao ili kuweza kufikia lengo la Morogoro kupandishwa hadhi ya kuwa jiji.

Chonjo amesema hayo wakati akizindua mapipa ya kuhifadhia taka. Hafla iliyoambatana na ziara fupi ya kufanya usafi katika soko la Manzese, Manispaa ya Morogoro.

Hata hivyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga amesema kuna haja ya kuandaa mashindano ya usafi katika kata zote za Manispaa ya Morogoro ili kuweza kubaini kata ambazo ni changamoto hasa katika suala zima la usafi.