Madereva wapigwa msasa

0
173

Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani Kanda ya maalum ya Dar es salaam, Nuru Selemani amewasisitiza madereva kuwa makini wanapokuwa barabarani ili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika.

Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa kutoa vyeti kwa madereva wa malori, madereva wa magari ya kubeba wagonjwa pamoja wale wa kampuni mbalimbali waliohitimu mafunzo yao ya udereva, Kamanda Nuru pia amewataka madereva hao kuzingatia sheria wawapo barabarani.

Mafunzo yaliyotolewa kwa madereva hao yameandaliwa kwa ushirikiano wa kampuni za AAI, FIA, MICHELIN na ASAS.